Shirikisho la soka duniani Fifa limetoa orodha mpya ya viwango vya soka duniani baada ya kuchezwa kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018, Kenya na Tanzania zikishuka zaidi ya hatua 10 kwenye orodha hiyo..
Ujerumani bado wanaongoza wakifuatwa na Brazil na Ureno.
Wakati kwa viwango vya Afrika, Tunisia ikirudi kileleni mara baada ya kupita miaka 15 toka kufanya hivyo.
Lakini wakati Tunisia ikifanya hivyo, nchi za Afrika Mashariki yaani Kenya na Tanzania zimeporomoka zaidi. Tanzania inashikilia nafasi ya 136 sasa baada ya kushuka nafasi 11, Kenya nayo imeshuka nafasi 14 hadi nafasi 102. Wakati wenzao wakivurunda, nchi nyengine za Afrika Mashariki yaani Burundi imesalia nafasi ya 129, Uganda ikapanda hatua moja hadi nafasi ya 70
Katika mechi za kirafiki ambazo Harambee Stars walicheza hivi majuzi, walilazwa 1-0 na Thailand baada ya kuchapwa 2-1 na Iraq mjini Basra.
Malawi imeshuka nafasi moja hadi nambari 117 ambapo inafuatwa katika nafasi ya 118 na Rwanda ambao bado walishikilia nafasi hiyo katika orodha iliyotangazwa awali.
DR Congo wamepanda nafasi 7 hadi nafasi ya 35.
Afrika, Tunisia wanaongoza wakiwa nafasi ya 28 duniani baada ya kupanda hatua 3 wakifuatwa na Misri walio nafasi ya 30 dunian


Hivi ndivyo msimamo wa 10 wa viwango vya Afrika ulivyo kwa sasa (Vya Dunia kwenye mabano);
1. Tunisia (28)
2. Egypt (30)
3. Senegal (32)
4. Democratic Republic of Congo (35)
5. Nigeria (41)
6. Cameroon (42)
7. Morocco (48)
8. Ghana (52)
9. Burkina Faso (55)
10. Ivory Coast (61)

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.