Mshambuliaji wa zamani wa barcelona Neymar ambaye kwa sasa anakipiga PSG ya ufaransa jana baada ya mechi ya UEFA dhidi ya Anderletch ya ubelgiji Akiri kuwa anampango wa kumsaidia Mbappe afike levo za messi.
Mbappe ambaye ndani ya dakika ya tatu tu ya mchezo aliweza kuipatia PSG bao la kuongoza pia kumpatia pasi nzuri cavani na kufunga bao la pili kabla ya mapumziko,amekuwa moto wa kuotea mbali huku akiiwezesha psg kushinda michezo yake yote mitatu ya UEFA makundi.
Neymar alisema "Nitamsaidia Mbape kuwa Bora zaidi kama messi alivyonisaidia nikiwa barcelona,mbappe ni rafiki yangu"
Ikumbukwe kuwa mbappe ameweka rekodi ya kuwa nyota kinda wa kwanza kufunga mabao mengi Katika mechi za UEFA akiwa na umri wa miaka 18 tu.
Post a Comment
Post a Comment