Hizi Ndio kumbukumbu zangu za visa za Madenge sijui na wenzangu mnakumbuka zipi?

1. Madenge Darasani kwao alikuja mwalimu mpya wa kike. Akauliza swali 2+2= ? Madenge kama kawaida yake akanyoosha mkono Mwalimu akamchagua Madenge basi Madenge akajibu Mwalimu hiyo Rahisi ni 5(TANO) aliisema kwa nguvu zote... Mwalimu akamwambia Madenge umekosa ni 4 basi Madenge akajitetea Mwalimu mie nilikuwa nakujaribu tu kuona wewe Kweli Mwalimu au umekuja kututania sasa ndio nimekubali wewe mwalimu mie najuwa kama ni 4 endelea kufundisha kumbe unafaa... 

2. Madenge katoroka shule kamuaga Mwalimu amefiwa na Mjomba wake. Mwalimu baadae ikabidi aende kwa kina Madenge akamkuta Baba yake Madenge ameketi anasikiliza Radio mbao pembeni Betri za National zengine zipo juwani...LOl! yule Mwalimu kufika Baba madenge poleni Yule Baba kwamshangao na kitu Gani? Mwalimu- Madenge kaaga amefiwa na Mjomba wake hajamaliza Madenge katokea 

Baba Madenge- we Kenge Mjomba yako yupi huyo amefariki?

Madenge- Baba kwani hujui Ankal Maiko Jaksoni amefariki .... Baba yake akamtowa nduki..


3. Ya tatu na ya mwisho kwangu ni hii.

Madenge alikuwa na mchezo wa kukojoa kitandani sasa Kurudi Baba yake kwa hasira kamtowa mbio wewe kila siku unakojoa kitandani sasa katika zile mbio Madenge anakimbia huku anasema haya tuone Kikojozi wa sasa na wazamani anani anambio sana? tehteh.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.