Hizi ndizo rekodi 10 pekee ambazo zimewekwa katika soka na hazitarajiwi wala kuzaniwa kama zitakuja kuvunjwa mpaka hapo kama watu wanavopenda kusemaga "Labda dunia ipinduke"

1. MAGOLI MENGI KUWAHI KUFUNGWA NA GOLI KIPA

Kazi ya goli kipa katika timu ni moja tu nayo ni kulinda goli lake ili kuzuia wapinzani wasifunge.Lakini pale golikipa anapojiongezea kazi ingine ya pili siku zote lazima liwe jambo la kusataajabisha sana,

Mkongwe mmoja ambaye ni raia wa Brazili ambaye naye kipindi chake alikuwa ni goli kipa aliishangaza dunia kwa kuweka rekodi ambayo mpaka kupinduka kwa dunia labda ndio kutaifanya rekodi iyo ivunjwe.

Rogerio Ceni ndie mlinda mlango aliyewai kufunga magoli mengi kuliko magoli kipa wote kuwai kutoa, ambapo anashikilia rekodi ya kufunga jumla ya magoli 131. Mlinda mlango huyo ndie anayeongoza kutimiza kazi ambayo haimuhusu yeye akiwa kama goli kipa ambapo alikuwa akitimiza kazi iliyopaswa kufanya na mshambuliaji.


Kipindi hicho akiwa anaichezea klabu ya Sao Paulo ya nchini kwao Brazili ambapo klabu hiyo ndiyo aliitendea kazi akiwa kama kocha baada ya kustaafu anatazamwa kuwa kipa hatari kuanzia katika majukumu yake kama kipa na kama mshambuliaji pia. Kipa anayemfata kwa kufunga magoli mengi ni Jose Luis Chilavert akiwa na magoli 71,magoli 60 nyuma ya R.Ceni.

R.Ceni amecheza mpira kwa muda wa miongo miwili na nusu sawa na mkongwe wa manchester united Ryann Giggs ambaye mpaka kustaafu kwake  alikuwa na magoli 111 huku akicheza sehemu ya ushambuliaji maisha yake yote ya soka.

2. MCHEZAJI ALIYEFUNGA MAGOLI MENGI KATIKA HISTORIA YA SOKA

Tukizungumzia maswala ya magoli wengi katika vichwa vyetu yanatujia majina makubwa kama Pelle, Ronaldo na Eusebio au hata Messi hawakaribii hata kidogo ukija katika swala la upachikaji magoli au kucheka na nyavu kama wanasoka wanavyopenda kusema.

JINA
MECHI
MAGOLI
MIAKA
Josef Bican
918
1468
1931-1956
Gerd Muller
1216
1461
1962-1983
Pelle
1375
1389
1956-1990
Arthur Friedenreich
1239
1329
1909-1935
Franz Binder
756
1006
1930-1949
Romario
1188
968
1985-2007
Eusebio
807
790
1957-1979
Puskas
754
746
1943-1966


3. TIMU ILIYOCHUKUA TAJI LA ULAYA MARA NYINGI MFULULIZO
Rekodi hii isiyoweza kuvunjwa mpaka dunia itakapopinduka imewekwa mnamo mwaka 1955-1960 na Real Madrid  walifanikiwa kubeba taji hilo mara tano mfululizo

Rekodi kama hii haiwezi kujirudia tena katika miaka ya hivi karibuni ambapo kila siku timu zinazidi kujiimarisha na kuwa imara zaid.

Madridi katika miaka mitatu iliyopita iliweza kufanikiwa kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo kitu ambacho kwa zaidi ya miongo miwili timu za ulaya zimeshindwa kufanya hivyo (kuchukua kombe hilo la mabingwa wa ulaya mara mbili mfululizo)

4.MECHI ILIYOHUDHULIWA NA MASHABIKI WENGI ZAIDI TANGU KUGUNDULIWA KWA SOKA DUNIANI.

Katika fainali ya kombe la dunia ya mwaka 1950 katika ya Brazili na uruguay iliyofanyika katika viwanja vya  amerika kusini ndiyo mechi inayoripotiwa kuhudhuriwa kwa miaka mingi zaidi duniani.

Mechi hiyo iliyopewa kwa jina "huge upset" ndiyo iliyohudhuriwa zaidi ambao mauzo rasmi ya tiketi yanaripotiwa kuwa 173,850 lakini waandishi wengi wanasema kuwa uwanjani kulikuwa na watu zaidi ya 210,000.

5. MAGOLI MENGI KUFUNGWA KATIKA MECHI MOJA
Amini usiamini, hii ndio haitokuja hata kukalibiwa kuja kuvunjwa, naamini hivyo maana ni rekodi ya aina yake. Ilikuwa mwezi oktoba mwaka 2002 katika mchezo kati ya AS Adema dhidi ya SO I'Emyrne ambapo walicheza mchezo wa kuwania ubingwa na mchezo huo kuisha kwa mabao 149-0.

Ilikuwa hivi, huko nchini Madagascar ambapo kulikuwa na mchezo wa kugombania ubingwa ambapo kwa sheria za michuano hiyo timu zinatakiwa kucheza nyumbani na ugenini katika mchezo wa fainali ambapo katika mchezo wa kwanza ambapo SO I'Emyrne ilikuwa nyumbani ikiikaribisha AS Adema na mchezo huo kuisha kwa sare ya 2-2. Lakini wachezaji wa timu iliyo nyumbani yaani Emyrne hawakulizishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo. Ambapo katika mchezo wa marudiano ili atakayeshinda hapo yatajumlishwa matokeo ya nyumbani na ugenini kisha mshindi kupatikana.

Lakini mchezo huo ulipoanza Emyrne ambao safari hii walikuwa ugenini wakaamua kuanza kujifunga wenyewe wakiamini kwa kuwa mwamuzi aliamua kuwakatili mchezo wa kwanza tena wakiwa nyumbani basi hata huu hawawezi kushinda kwa vili "mcheza kwao hutunzwa"

Basi kwa kauli hiyo wakaamua kujifunga wenyewe mpaka magoli yalipofikia AS Adema 149-0 Emyrne, matokeo yaliyomaanisha kuwa jumla ni 151-2.

Mchezo huo uliingizwa kwenye kitabu cha rekodi cha dunia maarufu kama Guinness Book of Records. Lakini pia mchezo huo haukuwaacha salama kocha wa timu hiyo iliyojifunga ambapo alifungiwa miaka 3 na wachezaji wake wanne ambao wao walifungia kushiriki soka mpaka mwisho wa msimu.

6. KUSHINDA KWAO NI KAMA MKOSI
Bila shaka mtu unaposkia kuhusu rekodi basi unatazamia rekodi hiyo inatazamiwa kuwaniwa. Lakini rekodi hii hakuna anayeitamani hata kidogo. Derby County ndio klabu pekee kushiriki ligi kuu ya soka na kumaliza huku ikiwa na ushindi mmoja tu.

Ilikuwa msimu wa 2007-2008 ambapo klabu ya nchini Uingereza ya Derby County iliweka rekodi mbovu kabisa kuwai kutokea mara baada ya kushiriki ligi na kufanikiwa kushinda mchezo mmoja tu dhidi ya Newcastle united na kufungwa michezo 29 (rekodi nyengine mbovu) na kusuluhu michezo 8 ambapo ilimaliza ligi ikiwa na alama 11 tu.



7. KUCHEZA MICHEZO MINGI
Bila shaka ikitajwa rekodi hii moja kwa moja utamfikiria haswa yule gwiji wa Brazili, Pelle ambaye juzijuzi alitoka kutimiza miaka 77, ambaye kipindi akiwa mwanasoka mpaka akatoka kwenye fani hiyo anaongoza kwa kucheza michezo 1375. Ni kweli ni michezo mingi lakini michezo hiyo inahesabiwa na ile akiwa kwenye akademi ya soka na ile ambayo haikuwa maalumu ambapo ukiichukua ile michezo inatambulika rasmi anakuwa na michezo 1115, ambayo ni namba kubwa japo so kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi.

Na badala yake rekodi hiyo inamdondokea yuleyule golikipa mwenye magoli mengi, Rogerio Ceni. Michezo 1217, inamfanya kuwa Ceni ndie mchezaji anayeshikilia rekodi ya kucheza michezo mingi toka dunia itokee.

8. KUTWAA TAJI LA ULAYA NA WACHEZAJI WAZAWA TU
Celtic ya nchini Scotland ilifanikiwa kutwaa taji la Ligi kuu ya mabingwa Ulaya mwaka 1967 huku kikosi chake kikihusisha wazawa tu. Celtic iliibamiza klabu ya Internazionale jumla ya magoli 2-1 na kufanikiwa kutwaa taji hilo la Ulaya huku kikosi chao kikijumuisha wazawa wa mtaa mmoja.

Kikosi cha msimu huo kilijumuisha wachezaji 15 ambapo wachezaji 14 wa kikosi hicho walizaliwa na kukulia nchini Scotland ambapo maeneo yao waliyoishi hayakuwa na umbali wa maili 10 na mchezaji mmoja pekee ndiye anatokea nje ya maili 20.

Kwa jinsi ya utandawazi wa leo inaonekana itakuwa ngumu kwa rekodi hiyo kuvunjwa kwa vile klabu nyingi na mashabiki wengi wanapenda kuona timu zao zikiwa na wachezaji wa bei kubwa.


9. KUFUNGA MAGOLI MENGI KWA NGAZI YA KIMATAIFA

Haya tena, mara nyingi sifa tunawapa akina Pelle na mwenzake Maradona na kuwaita ndio wafalme wa soka, sio kama nabisha lakini hao wote hawapo kwenye na rekodi hii. Mchezaji mwenye magoli mengi katika timu ya taifa ni Ali Daei ambaye ni raia wa Iran.

Ali Daei alitumia miaka 13 kuifungia timu yake ya taifa magoli 109 ambayo yanamfanya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kwa ngazi ya taifa. Daei pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea bara la Asia kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya huku akivichezea vilabu vikubwa vya Ulaya ambapo alishazichezea Hertha BSC na Bayern Munich.


10. MAGOLI MENGI KATIKA KOMBE LA DUNIA

Rekodi nyengine ni hii ambayo ni ngumu kuvunjwa kuliko hata kuuvunja upinde wa mvua.Just Fontaine alikuwa mwanasoka raia wa Ufaransa ambapo katika kome la dunia la mwaka 1958 alifunga magoli 13 ingawa timu yake haikufika fainali. Ambapo mpaka sasa rekodi inayoshikiliwa ya kufungwa magoli mengi katika mwaka mmoja wa kombe la dunia ni 16 mpaka michuano ikaisha lakini jamaa kwa michezo kadhaa halafu hajafika hata fainali lakini kafanikiwa kufunga magoli 13.

















Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.