Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji, Michy Batshuayi amekana taarifa zilizotolewa na chombo kimoja katika mtandao wa Twitter zikidai "Batshuayi ataka kujitangaza kujulikana kwamba ye mchezaji shoga"
Chombo hicho kinachotumia jina la @ChelseaDaily kinadai Batshuayi aliwaambia wachezaji wenzake kwamba yeye anafanya ushoga.
Kulikuwa na wachezaji kadhaa waliowai kujitambulisha kuwa ni mashoga ila wakifanya hivyo baada ya kuachana na soka la Uingereza ambalo ni soka lenye ushawishi duniani.
Kupitia mtandao huohuo wa Twitter, Batshuayi alijibu huku akitanguliza na vikatuni (emojis) za vicheko akionyeshwa kufurahishwa na kusema "Hata mama yako anajua kwamba hizo habari ni uongo" akiujibu huo mtandao uliomchafua.
Kumekuwa na harakati mbalimbali za vyama na watu wanaojihusisha na ushoga wakitaka kushawishi kwamba soka lisiwabague mashoga na wasagaji.
Post a Comment
Post a Comment