Ni mwaka mwengine bora kwa nyota raia wa Ureno ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambapo anafanikiwa kutwaa tunzo ya mchezaji bora wa mwaka zinazotolewa kwa jina la Ballon d'or. Kwa tunzo hiyo anaweza kuifikia rekodi iliyowekwa na mpinzani wake Lionel Messi ambaye naye amefanikiwa kutwaa tunzo hiyo.
Lakini pamoja na tunzo hiyo huenda kukawa na siri kubwa kwa mafanikio ya Ronaldo na namba 7, namba ambayo anaitumia hata kwenye jezi zake zote za timu ya taifa ya Ureno na klabu yake ya Real Madrid, lakini pia huenda mwaka 2017 ukawa mwaka bora kwake ambapo pia bado una namba 7 mwishoni mara baada ya kupata mafanikio mengi makubwa kwenye mwaka huo 2017,
Mwaka 2017 unamshuhudia Cristiano Ronaldo akifanikiwa kuisaidia Ureno kucheza kombe la dunia mwakani, lakini pia unamshuhudia akiisaidia klabu yake kubeba mataji matatu makubwa (ligi kuu Hispania, Klabu bingwa Ulaya pamoja na Klabu bingwa ya dunia).
Lakini pia katika ngazi ya familia, mwaka 2017 umemshuhudia Cristiano Ronaldo akifanikiwa kupata watoto watatu ambapo wawili wakiwa kama mapacha.
Lakini pia huenda hii ikawa tunzo kubwa ya mwisho kwa Cristiano kutokana, kwanza umri unamtupa mkono akiwa na miaka 33 sasa hivi, kushuka kwa kiwango sio kawaida ya Ronaldo kucheza mpaka mchezo wa 1 wa ligi kuu Hispania huku akiwa na magoli yasiyozidi matatu, lakini pia sababu ya mwisho ni huenda saba nyengine ikatokea mpaka mwaka 2027,hapo atakuwa na miaka 43.
Post a Comment
Post a Comment