Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameonekana kutokuwa na imani tena na mlinzi wa klabu hiyo, David Luiz.

Katika mkutano wa leo mchana ambao Conte amefanya na waandishi wa habari, aliulizwa juu ya mlinzi huyo raia wa Brazil, kwamba ni lini atarudi uwanjani kutoka katika majeruhi aliyonayo ya goti na je atakuwa na namba katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa awali, Conte akajibu "siwezi kusema ni lini atarudi, labda hilo aulizwe daktari, yeye ndiye anaweza kuwa na majibu kamili"

David Luiz anaonekana kutokuwa na uhakika wa namba kikosini hapo huku Andreas Christensen akionekana kuziba vizuri pengo la David Luiz aliye kwenye majeruhi akiuguza majeraha ya goti.

Chelsea inajiandaa na mchezo wa ligi kuu ambapo itamenyana na West Ham hapo kesho saa 15:30 katika uwanja wa London Stadium.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.