Kocha mwenye mbwembwe nyingi, Jose Mourinho huenda akajichimbia msingi ndani ya Manchester united, klabu anayoifundisha.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba, uongozi wa Manchester united upo kwenye mipango ya kutaka kumuongezea mkataba mwengine kocha huyo mreno.
Mourinho alisaini mkataba wa miaka mitatu ndani ya Manchester pindi alipokuwa anajiunga na klabu hiyo akichukua nafasi ya Luis Van Gaal, na sasa Man utd wamepanga kumpa mkataba mpya mara baada ya kuwepo tetesi kwamba kocha huyo anatakiwa na PSG.
Katika mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari kocha huyo alisema, "Nilifika Man utd nikitaka kuisaidia kubeba mataji, ambalo hilo nimelifanya msimu uliopita (alipobeb Europa, EFL na ngao ya hisani) lakini Uingereza unapozungumzia taji, basi unamaanisha Ligi kuu, na nina nia iyo ya kulitimiza hilo toka Ferguson alipofanya hivyo 2013"
Mourinho, wiki hii atakutana na kibarua kigumu ambapo atashuka uwanjani kumenyana na Newcastle united inayonolewa na Rafa Benitez, kocha wa zamani wa Liverpool, Chelsea na Real Madrid.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.