Nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi yamemkuta makubwa nchini kwao huko Amerika ya Kusini mara baada ya sanamu yake kuharibiwa tena.
Lionel Messi ambaye alifanikiwa kuisaidia timu yake ya taifa kwa kufunga magoli matatu (hat trick) iliyoisaidia timu yake kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani, sanamu yake iliripotiwa kuvunjwa sehemu ya juu na kubakisha sehemu ya miguu tu ambapo inaripotiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa tukio hilo kutokea kwa sanamu yake kuvunjwa.
Sanamu hiyo iliyojengwa katika mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires katika kitongoji cha Paseo de la Gloria ambacho baadhi ya sanamu za wanamichezo mashuhuri waliowai kutokea nchini humo zimejengwa hapo.
Post a Comment
Post a Comment