Mich batshuayiiii ama kama wanavyopenda kumuita Batman kwa mara ingine aiokoa chelsea mikononi mwa watford mchana wa leo baada ya kufunga mabao mawili akitokea benchi na kuiwezesha chelsea kupata point tatu muhimu kwao.
Katika mchezo ambao ulianza kwa chelsea kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Pedro akipiga shuti kali kumzidi gomez(kipa wa watford) lakini hali haikuwa shwari baada ya watford kusawazisha bao hilo sekunde chache kabla ya mapumziko.
kipindi cha pili kilianza kwa watford kuzidi kuisumbua ngome ya chelsea huku kocha antonio conte akionekana kuwa asiye na furaha kwa kile walichokuwa wanakifanya wachezaji wake.
Watford walipata bao la pili na lakuongoza ndani ya lisaa limoja la mchezo .
Kocha wa chelsea alifanya mabadiliko na kumtoa Morata na kumuingiza Batshuayi dakika ya 58 ya mchezo.Batshuayi hakufanya makosa na kufunga bao la kusawazisha na katika dakika za lala kwa buriani 95+ akatupia mkwaju wa nne ambao uliwaua kabisa watford.
Post a Comment
Post a Comment