Huenda hii ikawa habari mbaya zaidi kwa mashabiki wa soka haswa wa Chelsea, mara baada ya taarifa zilizotolewa na chombo kimoja barani Ulaya zikidai kuwa Eden Hazard amegoma kusaini mkataba mpya kwa sasa labda mpaka msimu huu ukiisha.

Taarifa zinadai kwamba Chelsea ipo tayari kumuongezea nyota huyo mkataba ambapo mkataba wake wa sasa unaisha 2020 na Chelsea ipo tayari kumlipa paundi 300,000 kama mshahara kwa wiki ingawa nyota huyo pia amekuwa akihusishwa kutakiwa na Real Madrid ambayo kocha wake Zinedine Zidane anaonekana kuwa na mahaba naye.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte alipoulizwa kuhusu mustakabari wa Hazard na kipa Thibaut Courtois ambaye naye amegoma kusaini mkataba mpya mpaka mwisho wa msimu alisema "Ni vyema kuwa na moja ya magolikipa bora duniani kwa sasa. Lakini pia kuwa na Hazard. Naamini kila mtu anaujua ubora wake"

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.