Timu ya taifa ya Zanzibar imeikung'uta timu ya Rwanda katika michuano ya Cecafa huko nchini Kenya kwa mabao 3-1.
Alianza Mudathir akiifungia timu yake goli la kuongoza dakika ya 34 na kuifanya Zanzibar kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, Rwanda walichomoa katika dakika ya 47 kupitia kwa Hakizimana na matokeo kuwa 1-1.
Dakika 52 ya nyota wa Zanzibar, Mudathir akaifungia tena goli la pili na kisha Kassim kuifungia goli la tatu katika dakika ya 86 na kufanya mpira kuisha kwa ushindi wa Zanzibar wakishinda 3-1.
Post a Comment
Post a Comment