Miezi michache baada ya aliyekuwa kocha wa The foxes ama Leicester city Muitaliano Claudio Ranieri maarufu kama "The tinker man" kutimuliwa kikosini hapo huku wengi wakidhani kuwa ilikuwa ni bahati tu kwa leicester city kutwaa ubingwa wa uingereza msimu wa 2015/16 chini ya kocha huyo,mapya yaibuka huko ufaransa yakidhibitusha kuwa muitaliano huyo hakubahatisha pindi alipokuwa leicester.
Muitaliano huyo alikubali kujiunga na klabu ya NANTES ya Ligi kuu ya ufaransa maarufu kama Ligue 1,klabu ambayo ilikuwa na misimu mibaya mingi ya nyuma na licha ya kumpa kibarua hicho Ranieri lakini uongozi wa klabu hiyo haukuwa unategemea makubwa.Kazi kubwa aliyopewa muitaliano huyo ilikuwa ni kuhakikisha timu haishuki daraja huku ikikumbukwa kabla ya ujio wa muitaliano huyo,msimu uliopit,chupu chupu washuke daraja..
Msimu mpya wa 2017/18 Ranieli aendeleza maajabu ya Leicester na baada ya mechi 10 tu kuchezwa kwenye ligi hiyo,NANTES wanashika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 20,pointi 6 nyuma ya vinala PSG.
Maswali mengi yanazidi ulizwa,je maajabu ya Leicester yanajirudia tena msimu huu?
Ikumbukwe,msimu mmoja kabla ya The foxes kuchukua ubingwa,ilibakia kidogo washuke daraja kama Nantes,historia kujirudia?
Majibu ya maswali haya tutayapata mwisho wa msimu huu.
Post a Comment
Post a Comment