
ambao Chelsea watakuwa nyumbani London, kocha wa timu hiyo Antonio Conte ametoa neno akiwa katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alipoulizwa juu ya nyota wa Roma amabaye kocha huyo amekuwa akimfukuzia kwa muda mrefu Radja Nainggolan ambaye usiku wa leo anategemewa kuwepo katika timu hiyo, Conte alisema "Radja ni mchezaji wa Roma kwa sasa, na bado ana mkataba huko, naliheshimu hilo"
Ukiachana na wababe hao, mchezo mwengine utakuwa baina ya Manchester united iliyo chini ya kocha Mourinho itamenyana na mabiingwa wa msimu uliopita wa nchini Ureno, Benfica. Ambapo mchezo huo ni wa kundi A huku Manshetani Wekundu wakiongoza kundi hilo kwa kushinda michezo yote miwili. Mchezo huo ni wa Kundi A.

Michezo mingine ukiachana na hao wababe wa nchi ya Malkia;
Qarabag vs Atletico Madrid-Kundi C
Anderlecht vs PSG-Kundi B
Bayern Munich vs Celtic-Kundi B
Barcelona vs Olympiacos-Kundi D
CSKA Moscow vs Basel-Kundi A
Juventus vs Sporting CP-Kundi D
Michezo hiyo itachezwa mishale ya saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Kasoro mechi ya Qarabag vs Atletico Madrid ndo itaanza saa 1:45 usiku.
Post a Comment
Post a Comment