Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ni mchezaji mwenye mafanikio sana barani Ulaya na duniani pia ambapo kwa sasa yeye pamoja na Lionel Messi ndio kama watawala wa dunia ya soka.
Lakini je unaijua safari ya maisha ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo? unajua ni yapi kayapitia mpaka kuwa na kiwango bora?
Hapa nakuletea historia fupi inayomhusu ambapo imekuwa ikisambaa mitandaoni kwa sana.
"sawa mimi ni mchezaji bora lakini mafanikio yangu yote yasingetokea kama asingekuwepo Alberto Fantrau" alisema Cristiano Ronaldo katika hafla ya kukabidhiwa tunzo ya mchezaji bora duniani.
Baada ya Ronaldo kuna wengi walijiuliza, Alberto Fantrau ni nani? na alifanya nini kuwa sababu ya mafanikio ya nyota kama Ronaldo?
Alberto Fantrau alikuwa ni mchezaji wa zamani ambaye alishawai kucheza klabu moja na Cristiano Ronaldo.
Siku moja wakufunzi wa klabu ya Sporting Lisbon walitoa ofa kwamba atakayefunga magoli mengi ndiye atakayebebwa kwenda kujiunga na Sporting Lisbon.
Timu ya akina Ronaldo ilifanikiwa kushinda 3-0 huku magoli yakifungwa na Alberto Fantrau pamoja Cristiano Ronaldo wakati katika goli la tatu ndilo linaifanya dunia imfaidi Ronaldo, unajua ilikuwaje?
Alberto Fantrau alimpiga chenga mpaka kipa na kubakiwa na nyavu tu ili afunge lakini badala ya kufunga goli hilo ili achukuliwe na Sporting Lisbon lakini Fantrau akampasia Cristiano Ronaldo na kufunga.
Baada ya mchezo huo Ronaldo alimfta Fantrau na kumuuliza kwanini hakufunga mwenyewe, Fantrau alijibu "kwa vile naamini wewe unajua kuliko"
Toka hapo Fantrau aliachana na soka na sasa anamiliki majumba na magari, vitu ambayo Fantrau alishawai kukiri kwamba kanunuliwa na Cristiano Ronaldo kama asante yake.
Wiki hii kunaenda kufanyika shughuli ya kumtangaza tena nyota bora dunuani ambapo tatu bora ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi pamoja na Neymar.


Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.