Kiungo ghali zaidi klabuni Manchester united, Paul Labile Pogba kumbe ni shabiki wa klabu ya Arsenal ambapo leo jioni klabu hizo zitamenyana katika raundi ya 15 ya ligi kuu Uingereza.
Pogba alipohojiwa na chombo kimoja cha habari uko nchini Uingereza alisema "wakati nikiwa mdogo, kulikuwa kuna klabu kadhaa nazitazama ila nilikuwa naiangalia sana klabu iliyokuwa na wafaransa wengi haswa nilikuwa namtazama sana Thierry Henry. Nilikuwa shabiki wa Arsenal, japo sio yule mwenye mapenzi sana, ila nilikuwa naipenda"
Pogba usiku wa leo anatarajiwa kuiongoza Manchester united kushuka dimbani wakikaribishwa na Arsenal katika mchezo mgumu ambapo klabu zote zinahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri.
Michezo mingine EPL;
Chelsea vs Newcastle (saa 15:30)
Brighton vs Liverpool (saa 18:00)
Stoke city vs Swansea (saa 18:00)
Everton vs Huddersfield (saa 18:00)
West Brom vs Crystal Palace (saa 18:00)
Watford vs Tottenham (saa 18:00)
Leicester vs Burnley (saa 18:00)
Post a Comment
Post a Comment