Mchezo wa mapema katika ligi kuu Uingereza leo jumamosi ulikuwa ni kati ya Chelsea iliyokuwa nyumbani ikiikaribisha Newcastle united iliyopanda daraja msimu huu ikiwa chini ya kocha Rafa Benitez ambaye alishawai kuifundisha Chelsea.

Mchezo ulianza kwa Newcastle kuonyesha umahiri wake katika kushambulia kabla ya Gayle kuifungia klabu yake bao la kuongoza na kufanya matokeo kuwa Chelsea 0 wakati Newcastle 1.

Dakika kadhaa baadae Eden Hazard akachomoa goli kabla ya Morata kufunga kwa kichwa akipokea pasi murua kutoka kwa Mnigeria, Victor Moses. Na kufanya mpira kwenda mapumziko Chelsea ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilikuja na goli moja tu alilofunga Eden Hazard kwa njia ya penati na matokeo kuwa 3-1.

Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea kuwa na alama 32 sawa na Manchester united anayecheza usiku wa leo saa 20:30 dhidi ya Arsenal.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.