Bado ubabe wa kocha Jose Mourinho unaendelea kwa Arsene Wenger, ambapo usiku wa leo ameshuhudia klabu yake ya washika bunduki ikigaragazwa mabao 1-3 huku Arsenal akiwa nyumbani.

Alikuwa Antoinne Valencia aliyefungua karamu ya magoli huku Jese Lingard akifatia baada ya Man utd kutumia makosa ya mlinzi Mustafi na kufanya matokeo kuwa Arsenal 0 huku Man utd 2 mpaka timu hizo zikienda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kushambulia kwa kasi na kutengeneza nafasi nyingi ili iweze kupata matokeo huku ikipata goli lake la kwanza likifungwa na Alexzander Lacazette kabla tena ya Jese Lingard kufunga tena akipokea pasi kutoka kwa Paul Labile Pogba na kufanya matokeo kuwa 1-3.

Lakini pia wakati mpira ukiwa unaendelea, nyota Paul Pogba alimchezea rafu Bellerin akimkanyaga chini ya paja na mwamuzi kumpa kadi nyekundu inayomaanisha atakosa michezo kadhaa ikiwemo unaofata dhidi ya Manchester city utakaochezwa desemba 10.

Matokeo mengine EPL;
Chelsea 3-1 Newcastle
Brighton 1-5 Liverpool
West Brom 0-0 Crystal Palace
Leicester 1-0 Burnley
Watford 1-1 Tottenham
Stoke city 2-1 Swansea
Everton 2-0 Huddersfield

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.