Klabu ya Chelsea imeungana na klabu nyengine katika timu zilizofuzu kucheza ligi ya mabingwa Ulaya katika hatua ya 16-Bora.

Chelsea imeifunga Qarabag usiku wa leo mabao 4-0 na kufikisha alama 11 na kuongoza kundi C akifuatiwa na AS Roma ambaye yeye atacheza dhidi ya Atletico Madrid usiku wa leo.

Alianza raia wa Ubelgiji, Eden Hazard kuifungia Chelsea goli la kwanza kwa mkwaju wa penati kabla ya Willian kufunga goli la pili na Cesc Fabregas kufunga tena kwa penati baada ya Willian kufanyiwa madhambi na mwisho goli la nne kufungwa na Willian kwa shuti la mbali.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufuzu kucheza hatua ya 16-bora ikiungana na PSG, Real Madrid, Tottenham, Besiktas, Manchester city na Bayern Munich.

Wakati hayo yakitokea kwa mabingwa watetezi wa Uingereza, Chelsea huko nako kwa akina CSKA Moscow wanachoombea kwa sasa ni Man utd kushinda katika mchezo dhidi ya Basel ili CSKA Moscow awe na matumaini ya kufuzu.

Mara baada ya CSKA Moscow kuifunga Benfica katika mchezo wa wapema leo, CSKA Moscow wamefanikiwa kupanda kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya pili na kufikisha alama 9 katika kundi A linaloongozwa na Man utd yenye alama 12 huku Basel akishika nafasi ya 3 akiwa na alama 6.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.