Nyota wa klabu ya Everton na raia wa Senegal, Oumar Niasse amepewa adhabu na chama cha soka cha nchini Uingereza, FA.
Niasse ameadhibiwa kutokana na kujiangusha katika mchezo dhidi ya Crystal Palace ambapo refa aliweka penati na Leighton Baines kufunga mkwaju huo na matokeo kuwa 1-0 ingawa mpira uliisha kwa suluhu ya 2-2.
Niasse amepewa adhabu ya kufungiwa michezo miwili ambapo atazikosa Southampton na West Ham katika ligi kuu.
Kabla ya msimu kuanza chama cha soka cha Uingereza, FA kilitambulisha sheria mpya kwa mchezaji atakayeonekana amejiangusha haswa kwenye eneo la hatari na sheria imeanza kuhukumiwa kwa Niasse akiwa ndie mchezaji wa kwanza kukutana na rungu hilo.
Post a Comment
Post a Comment