Ni usiku wa mabingwa Ulaya, na kila mtu alitegemea kupata kile ambacho alikitegemea usiku huu.
Barcelona nayo tayari 16 bora
klabu hiyo imetimiza klabu nane ziluzofuzu katika hatua ya 16 bora baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Juventus na hivyo kufuzu ukiwa umebaki mchezo mmoja katika kundi.

PSG yafanya tulichokitegemea
Katika uchambuzi wa michezo hii, nilikwambia utamu wa mchezo huu utakuja kutokana na safu ya ushambuliaji ya PSG ikiwa imekamilishwa na nyota kama Mbappe, Neymar na Cavani na katika mchezo huo, PSG ilishinda kwa mabao 7-1 huku magoli yakifungwa na Neymar aliyefunga mara mbili, Edinson Cavani naye kafunga mara mbili wakati magoli mengi yakifungwa na Mbappe, Dani Alves na Marco Verrati.

Kwa magoli hayo ya Neymar na Cavani yanafanya kuwa nyuma ya Cristiano Ronaldo anayeongoza kwa ufungaji akiwa na magoli 8 huku wao wakiwa na magoli 6.
Man utd yacheleweshwa kufuzu
Man utd walitakiwa kupata alama moja tu ili kuweza kufuzu kucheza hatua ya 16 bora, lakini jana FC Basel ikaichelewesha klabu hiyo kuweza kufuzu mara baada ya kuifunga goli 1-0, goli likifungwa na Lang. Ingawa ni kama kumchelewesha tu kufuzu kutokana na msimamo wa kundi lao ulivyo.

Simeone mguu ndani, mguu nje 16-Bora
Klabu ya Atletico Madrid imerudisha matumaini ya kuweza kufuzu kucheza hatua ya 16 bora mara baada ya jana kuitungua klabu ya As Roma kwa magoli 2-0, magoli yakifungwa na Antoinne Griezman na Gameiro na kuifanya klabu hiyo kurudisha matumaini, na kama itataka kufika hatua ya 16 bora basi ni lazima aifunge Chelsea katika mchezo unaokuja ugenini katika uwanja wa Stamford Bridge wakati huku AS Roma afungwe na Qarabag.

Matokeo mengine;
Anderlecht 1 vs 2 Bayern Munich
Sporting CP 3 vs 1 Olympiacos
Anderlecht 1 vs 2 Bayern Munich
Sporting CP 3 vs 1 Olympiacos
Post a Comment
Post a Comment