Katika mchezo wa jana katika klabu bingwa Ulaya kati ya Juventus dhidi ya Barcelona uliochezwa mjini Turin na kuisha kwa suluhu ya kutokufangana kulizuka mjadala mkubwa mara baada ya mchezo huo kuisha.
Messi ambaye katika mchezo huo alianza akiwa nje ambapo mara ya mwisho kwa mchezaji huyo kuanzia nje ilikuwa miezi 13 kabla ya kuingia dakika ya 56 akichukua nafasi ya kinda Deulefou.
Lakini mzozo na mijadala ilianza kuzuka pale mpira ulipoisha na nyota huyo wa Argentina kuonekana akiwa na wachezaji wa Juventus.
Messi alimfata Dybala na kuanza kuongea nae na kuonekana pia akiwa na nyota mwengine wa Juventus, Gonzalo Higuain tena wakiwa wanacheka katika njia ya kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.
Picha hizo zimeibua mzozo sana haswa nchini Argentina ambapo huko ndipo wanapotokea nyota hao.
Post a Comment
Post a Comment