Nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar dos Santos ambaye anashika rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani ameonyesha mapenzi yake kwa mpiga mgumi raia wa Marekani, Floyd Mayweather.

Neymar ameonyesha mapenzi hayo kwa mwana masumbwi huyo katika mchezo wa klabu yake ya PSG ilipomenyana na Celtic jana usiku katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Wakati wachezaji wanatoka vyumbani kuelekea uwanjani, nyota huyo alivaa koti lililoandikwa jina la mpiganaji Floyd Mayweather ambapo hiyo ilionekana kama mchezaji huyo alitaka kuonesha mapenzi yake kwa mwanamasumbwi huyo tajiri duniani.

Na katika mchezo huo Neymar akafunga mara mbili na kuwa mchezaji wa pili wa kibrazili mwenye magoli mengi kwenye michuano hiyo akiwa na magoli 27 huku kundi hilo likiongozwa na Ricardo Kaka mwenye magoli 30. PSG ilishinda 7-1 katika mchezo huo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.