Nyota wa zamani wa Real Madrid na Manchester city, Robinho amekutwa na hatia katika kesi ya unyanyasaji wa kingono na kutupwa gerezani miaka tisa.
Robinho mwenye miaka 33 kwa sasa ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa amekutwa na hukumu hiyo mara baada ya kuwa na mashtaka kwamba mwaka 2013 alihusika kumbaka mwanamke raia wa Albania.
Robinho ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Atletico Mineiro aliwai kung'aa katika kikosi cha Manchester city akiwa mmoja wa wachezaji ghali kununuliwa na tajiri Sheikh Mansour wakati tajiri huyo alipomwaga pesa katika klabu hiyo baada ya kuinunua.
Robinho ameingia katika kesi hii muda mfupi baada ya nyota na msanii wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kuhukumiwa kifungo miaka miwili kwa kesi ya kuua bila kukusudia.
Post a Comment
Post a Comment