Kocha mpya wa klabu ya nchini Uingereza, David Moyes amewaambia mashabiki wa klabu hiyo atawapa cha kuimba.
Mashabiki wa West Ham walisikika wakiimba "haufai katika timu hii" katika mchezo wa klabu hiyo ilipomenyana na Watford katika mchezo wa ligi kutoa ujumbe kwa kocha huyo kwamba aondoke klabuni hapo maana timu haimfai.
Alipoulizwa kocha huyo kuimbiwa maneno kama hayo tena katika mchezo wake wa kwanza alisema;
"nadhani mashabiki hawapaswi kuwa hivi, inatakiwa waungane na sisi ili tufanye vizuri" amesema kocha huyo ambaye alishawai kuzifundisha klabu za Man utd na Real Sociedad bila mafanikio.
"naamini nitawapa nyimbo nzuri ya kutushabikia pale klabu itakapokuwa inafanya vizuri, lakini kwa matokeo haya na mchezo huu wa sasa sihitaji kulaumiwa maana ndio mchezo wa kwanza kwangu, na bado nina nafasi ya kuwaonyesha mengi mazuri" alisema David Moyes ambapo wiki hii ataiongoza klabu yake kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Leicester city katika uwanja wa London Stadium, West Ham wakiwa nyumbani.
Post a Comment
Post a Comment