Ni usiku mwengine mtamu kwa kocha wa Manchester city, Pep Guardiola mara baada ya kupata ushindi muhimu jioni ya leo ikitoka nyuma na kushinda 2-1.

Alikuwa ni Ogbonna aliyeanza kufungua karamu ya magoli ambapo aliifungia West Ham goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na West Ham iliyochini ya kocha David Moyes kuwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili, ilikuwa ni zamu kwa Manchester city mara baada ya kuchomoa kupitia kwa mlinzi Otamendi na kufanya matokeo kuwa 1-1, lakini wakati mpira ukielekea kuisha David Silva aliifungia bao la ushindi klabu yake na kuifanya Manchester city kumaliza mchezo ikishinda 2-1.

Manchester city kwa ushindi huu unaifanya ifikishe alama 43 huku ikimuacha Manchester united inayoshika nafasi ya pili kwa alama nane.

Matokeo mengine EPL;
AFC Bournemouth 1-1 Southampton

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.