Ni usiku mtamu kwa klabu ya Benevento inayoshiriki ligi kuu ya Italia, maarufu kama Serie A lakini ni siku tamu zaidi kwa kipa wa klabu hiyo, Alberto Brignoli mara baada ya kufunga goli katika mchezo dhidi ya AC Milan leo jioni wakitoka nyuma kwa 2-1 na kuchomoa goli na kuwa 2-2.
AC Milan iliyokuwa chini ya kocha wao mpya Genaro Gattuso ilianza kwa kuongoza kwa mabao 2-1 kabla ya kipa Brignoli kuipatia goli klabu yake akifunga kwa kichwa, ambapo hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa mlinda mlango kufunga toka alipofanya hivyo Massimo Taibi mnamo mwaka 2001.
Kwa goli hilo la kipa huyo linaifanya klabu hiyo ya Benevento kupata alama yake ya kwanza katika ligi hiyo wakiwa walipoteza michezo yao yote kabla ya mchezo wa leo.
Wakati huohuo, klabu ya Inter Milan imefanikiwa kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Italia, Serie A mara baada ya kuibamiza klabu ya Chievo magoli 5-0.
Matokeo mengine Serie A (Jana na Leo);
Bologna 1-1 Cagriali
Fiorentina 3-0 Sassuolo

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.