Siku ya leo jumapili katika viwanja vya shule ya sekondari Azania jijini Dar es Salaam kutakuwa na michezo ya fainali katika mchezo wa Baseball ambapo itafanyika jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa ikizikutanisha klabu mbalimbali kutokea katika shule za sekondari katika mikoa tofauti tofauti kama mkoa wa Dodoma, Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam kama wenyeji.
Timu ya shule ya Azania itakuwa kama wenyeji wa mashindano kutokea mkoa wa Dar es Salaam lakini pia ikijumuisha na klabu zilizoibuliwa mwanzoni katika kliniki ya Baseball ikiwa inafika Tanzania haswa mkoa wa Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya Baseball ambayo yamepewa jina la "5th Tanzania Koshien Baseball Championship" ambayo yalifunguliwa na mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Sanaa na Michezo, Mh. Julliana Shonza (Mb) ambapo aliyafungua mashindano hayo tarehe mosi desemba.
Na leo ndio itachezeka michezo ya fainali ambapo mashindano hayo yatakuwa chini ya usimamizi wa wakufunzi kutoka Japan ambako huko ndiko chimbuko lake.
Post a Comment
Post a Comment