Kocha wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane jana alishuhudia timu yake ikitoka suluhu na klabu ya Athletic Club, sare ya kutokufungana.
Baada ya mchezo huo alifanya mkutano mfupi na waandishi wa habari na alipoulizwa mwenendo wa timu yake huku akiachwa alama 8 na Barcelona iliyo kileleni.
"kinachotufanya tuwe nyuma ya Barca kwa alama zote hizo kwa vile hatufungi" alisema Zidane.
"imekuwa tofauti na msimu uliopita, tulikuwa tunaweza kufunga hata dakika za mwisho, ila msimu huu haitokei hiyo"
"najua hii itaponywa kwa njia moja tu, ya kupambana na kufanya mazoezi zaidi"
Alisema Zidane ambapo mpaka sasa ikiwa imeshachezeka michezo 14, Real Madrid ikiwa na alama 28 ikiwa nafasi ya nne wakati Barcelona ipo kileleni huku ikiwa na alama 36.
Michezo mingine La Liga;
Barcelona 2-2 Celta Vigo
Atletico Madrid 2-1 Real Sociedad
Sevilla 2-0 Deportivo la Coruna
Post a Comment
Post a Comment