Klabu ya Chelsea ambayo ina makao magharibi mwa jiji la London imeamua kusitisha mpango wake wa kutanua uwanja wao unaoitwa Stamford Bridge.
Chelsea ambayo ilifikiria kuutanua uwanja wao ambao kwa sasa unachukua watazamaji 41,000 na huku ukiwa uwanja mkongwe ambapo mwaka 1877 ndio ulijengwa na kutumika na klabu ya London Athletic Club kabla ya mwaka 1905, pale ilipoanzishwa klabu ya Chelsea yenye jina la utani "The Blues" ilipoanza kuutumia uwanja huo.
Bodi ya Chelsea ikiongozwa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Bruce walikutana ambapo Marina Glanovskaia nae akiwa mmoja wapo walipojadili kuhusu mpango huo wa kuutanua uwanja kutoka siti 41,000 za watazamaji mpaka kufikia 60,000 ambapo bajeti yake ili uwanja huo ukamilike ni paundi milioni 500.
Kikubwa kilichoamuliwa katika kikao hicho ni kwamba uwanja wa Stamford Bridge utaanza kujengwa rasmi msimu wa 2021-2022 na ikakadiliwa huenda Chelsea ikarudi uwanjani hapo msimu wa 2024-2025.
Ambapo kwa kipindi chote ambapo Stamford utakuwa unajengwa, huenda Chelsea ikautumia uwanja wa Wembley.
Post a Comment
Post a Comment