Mshambuliaji wa Ubelgiji ambaye anaichezea klabu ya Manchester united, Romelu Lukaku ameiongoza vyema timu yake ya taifa ikitoa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico.

Walianza Ubelgiji kwa bao safi la Lukaku akifunga akipokea pasi kutoka kwa Mertens kabla ya Luzano wa Mexico kusawazisha na matokeo kuwa 1-1. Baadae kidogo Lukaku akafunga tena akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Mertens kabla tena ya Luzano kusawazisha tena na matokeo kuwa 2-2.

Bila kutarajiwa Guardado wa Mexico akaifungia tena Mexico bao jengine na kuwafanya Ubelgiji waumie vichwa kabla ya nyota wa klabu ya Chelsea anayefukuziwa kwa karibu na Real Madrid, Eden Hazard kusawazisha na kufanya matokeo kuwa sare ya mabao 3-3.

Wakati hayo yakitokea, timu ya taifa ya Ufaransa ilimkamata kibonde na kumfunga mabao 2-0, magoli ya Ufaransa yakifungwa na Antoinne Griezman na Olivier Giroud.

Huku Ujerumani nae akisuluhu kwa sare isiyo ya magoli ya 0-0 dhidi ya Uingereza waliokuwa wakitumia mfumo wa refa wa video kwa mara ya kwanza katika uwanja wao wa jijini London, Wembley Stadium.

Poland nae akamaliza mchezo kwa suluhu isiyo ya magoli ya 0-0 dhidi ya Uruguay.

Mchezo mwengine wa kirafiki unaoendelea ni kati ya Ureno iliyombele kwa mabao 2-0 dhidi ya Pakistan.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.