Ulikuwa ni mchezo mgumu wa kugombania kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018, kati ya Sweden iliyokuwa inacheza bila ya mfungaji wake bora wa muda wote Ibrahimovic ikimenyana na Italia ambapo mchezo umeisha kwa Sweden kutoka kifua mbele kwa kushinda 1-0, goli likifungwa na Johannsen.
Matokeo ambayo ni magumu kwa Italia kumfanya kuwa na asilimia kubwa kuweza kufuzu kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani ambayo itafanyika nchini Urusi.
Lakini kabla ya mchezo huo kuanza, kipa mkongwe wa Italia, Gianluigi Buffon alipohojiwa alisema "tukiwa tunaingia kwenye mchezo huu, tuna asilimia 50 ya uhakika kwamba tutafuzu. Na kama itatokea matokeo yakiwa vibaya basi nitastaafu rasmi" alisema kipa huyo mkongwe.
Post a Comment
Post a Comment