Klabu ya Borussia Dortmund imetangaza rasmi kuachana na kocha wake Peter Bosz kutokana na matokeo mabovu ambapo 'weekend' hii ameiongoza tena klabu hiyo kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Werder Bremen.
Bosz aliyeanza vizuri msimu huu akiwa ndio kakabidhiwa timu kutoka kwa Tuchel alianza vizuri mara baada ya kuongoza katika msimamo na kushika nafasi ya kwanza huku ikimuacha anayeshika nafasi ya pili kwa alama tano kabla ya kuanza kupata matokeo mabovu ambapo katika michezo nane iliyopita amevuna alama 3 tu akitoka sare michezo mitatu na kufungwa michezo 5 huku pia akishindwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Kocha Peter Stoger, aliyekuwa kocha wa FC Koln amechaguliwa kushika nafasi ya Bosz ambapo amepewa mamlaka ya kuifundisha klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu.
Post a Comment
Post a Comment