Raia wa Ufaransa, Olivier Giroud ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ameiokoa klabu yake kunusurika kipigo dhidi ya Southampton leo jioni ambapo Arsenal ilishafungwa goli 1-0 dakika ya tatu ya mchezo katika kipindi cha kwanza, goli likifungwa na Charlie Austin.
Kabla ya Olivier Giroud kuingia kuchukua nafasi ya Alexzander Lacazette na kufanikiwa kuchomoa goli hilo dakika ya 87 ya mchezo.
Kwa sare hiyo ya Arsenal inamfanya kufikisha alama 29 na kufanikiwa kupanda kutoka nafasi ya sita aliyokuwepo mara baada ya ushindi wa Tottenham jana na sasa Arsenal imerudi nafasi yake ya tano huku Tottenham akishuka mpaka nafasi ya sita.
Michezo mingine leo EPL;
Liverpool vs Everton (saa 17:15)
Man utd vs Man city (saa 19:30)
Post a Comment
Post a Comment