Leo ni siku nyengine tamu ambayo itakuwa huenda ndio wiki tamu na nzuri kuliko wiki zote toka ligi kuu Uingereza ianze.
Leo ni siku ya mechi za watani wa jadi (derby) nchini humo ambapo viwanja viwili jioni ya leo vitatimka vumbi pale ambapo timu vigogo wa jiji moja watakapocheza katika jiji lao.
Merseyside Derby
Watani wa jadi ambao mechi yao inakaribia kuanza ni kati ya Liverpool itakapomkaribisha Everton uwanjani Anfield ingawa wote wanatokea katika jiji moja la Merseyside.
Mchezo huo unategemewa kuwa mgumu zaidi kutokana na klabu hizo na nafasi zake katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Liverpool atataka ashinde ili apande kutoka nafasi ya nne mpaka ya tatu ambapo ataishusha Chelsea iliyotoka kupoteza mchezo wake jana dhidi ya West Ham, wakati kwa Everton imekuwa haina msimu mzuri wa maana hiyo itataka kuutumia mchezo huu kujiweka sawa na kurudi kwenye ubora wake.
Manchester derby
Huu ndio mchezo mwengine unaosubiriwa kwa hamu ambapo utachezwa mida ya saa 19:30 pale kwenye dimba la Old Trafford, Man utd akiwa nyumbani kuikaribisha Man city iliyo kwenye ubora wa hali ya juu ikiwa imecheza michezo 15 bila kupoteza huku ikitoka suluhu mchezo mmoja.
Kila timu itahitaji ushindi katika mchezo huu ambapo endapo Man utd wakishinda basi watapunguza pengo la alama dhidi ya vinara Man city kutoka alama 8 mpaka alama 5. Lakini pia kwa Man city watataka kushinda mchezo huu ili kuweka pengo kubwa la alama dhidi ya mtu wa pili ambaye ni Man utd kutoka alama 8 mpaka alama 11.
Je nani kuwa mtani wa kweli huko Uingereza?
Post a Comment
Post a Comment