Klabu ya Liverpool imetoka suluhu katika mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Everton kwa magoli 1-1, huku Mohammed Salah akizidi kujiweka kileleni katika ufungaji bora akiwa na magoli 13 akifuatiwa na Harry Kane mwenye magoli 12.

Katika mchezo huo, Liverpool ndio waliokuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa nyota wao hatari Mohammed Salah akifunga kwa ustadi mkubwa na mpaka mpira kwenda mapumziko Liverpool wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza, huku dakika kadhaa baada ya kutoka mapumziko kocha wa Liverpool akafanya mabadiliko akitoka Mohammed Salah na kuingia Roberto Firmino, mabadiliko ambayo yamelalamikiwa na mashabiki na wapenzi wengi wa Liverpool ambapo mara baada ya mabadiliko hayo baada ya muda Everton ikapata penati iliyopigwa na Wayne Rooney na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kusalia kwenye nafasi yake ileile ya 4 akiwa na alama 30 kwenye msimamo wa ligi kuu, akishindwa kuishusha Chelsea iliyopoteza jana dhidi ya West Ham ambao wao wanashika nafasi ya 3 wakiwa na alama 35.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.