Klabu ya Manchester city imeigaragaza klabu ya Manchester united kwenye uwanja wa Old Trafford kwa magoli 2-1 na kuvunja rekodi ya Arsenal ya kushinda michezo 14 bila kufungwa aliyoiweka msimu wa 2003-2004.
Man city ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa David Silva akifunga kwa guu lake la kushoto kabla ya dakika kadhaa baadae Rashford kuchomoa na kufanya mpira kwenda mapumziko zikitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko, Vincent Kompany akitoka nafasi yake ikichukuliwa na Iikay Gundogan huku kwa Man utd akitoka Marcos Rojo na nafasi yake kuchukuliwa na Victor Lindelof.
Lakini dakika kadhaa baadae Otamendi akaifungia tena Manchester city goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka mpira unaisha.
Kwa matokeo haya yanaifanya Manchester city kuongoza kwa tofauti ya alama 11 alizomwacha Manchester united mwenye alama 35 huku akishika nafasi ya pili, wakati Chelsea akishika nafasi ya tatu akiwa na alama 32 akifuatiwa na Liverpool anayeshika nafasi ya nne akiwa na alama 30, Arsenal nafasi ya tano akiwa na alama 29 huku Tottenham akishika nafasi ya sita.
Matokeo mengine EPL;
Southampton 1-1 Arsenal
Liverpool 1-1 Everton
Post a Comment
Post a Comment