Kiungo raia wa Croatia, Ivan Rakitic anayeichezea klabu ya Barcelona ameamua kutoa lake la moyoni juu ya nani bora kati ya Lionel Messi, anayecheza nae Barcelona na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliyetoka kushinda tunzo ya mchezaji bora Ballon d'or wiki iliyopita.
Rakitic alisema "sawa naheshimu ukubwa wa Ronaldo, ila anashindana na (Messi) mchezaji bora duniani"
Ronaldo alishinda tunzo ya Ballon d'or ambapo kwa kushinda tunzo hiyo ilimfanya aifikie rekodi ya Lionel Messi ya kubeba tunzo hiyo mara tano.
Messi jana aliisaidia klabu yake ya Barcelona kushinda ugenini kwa Villareal katika ushindi wa 2-0 ugenini huku goli la pili akifunga Messi na jengine kufungwa na Luis Suarez.
Lakini pia kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde kabla ya mchezo huo kuanza aliulizwa kuhusu nani alistahili kushinda tunzo hiyo, na kocha alijibu " sawa Ronaldo ameshinda, lakini kwa upande wangu naamini wachezaji bora wanapatikana hapa Barcelona, akianza Messi na wengine wanafata"

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.