Nyota wa klabu ya Liverpool, Mohammed Salah ambaye ni raia wa Misri ameshinda tunzo ya mchezaji bora kutoka Afrika, tunzo inayotolewa na chombo cha uandishi wa habari cha BBC.
Salah ameshinda tunzo hiyo akiwapiku nyota kutoka Chelsea raia wa Nigeria Victor Moses, raia kutoka Gabon anayeichezea Borrusia Dortmund, Pierre Aubameyang, Naby Keita anayeichezea RB Leipzig ya Bundesliga na Sadio Mane anayecheza nae Liverpool ambaye ni raia wa Senegal.
wakati hayo yakiendelea
Klabu ya Liverpool ambayo ndiyo anayochezea Salah kwa sasa imepangwa kukutana na FC Porto kutoka nchini Ureno katika hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa Ulaya ambapo droo hiyo imefanyika leo, huku Chelsea ikipangwa kucheza dhidi ya Barcelona, Manchester city akianza ugenini dhidi ya FC Basel, Manchester united dhidi ya Sevilla atakayeanza nyumbani wakati pia Tottenham atamenyana na Juventus.
Post a Comment
Post a Comment