Unamkumbuka Lous Van Gaal? yule kocha mholanzi aliyewai kuifundisha Manchester united kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho aliiyeichukua nafasi hiyo msimu huu. Sasa Van Gaal ametoka huko alipo na kumpiga dongo Mourinho. Unajua kasema nini?
"heri Manchester ile ya kwangu ilikuwa inaeleweka na inacheza mpira safi, kuliko hii ya sasa. Mpira wake unakera kuitazama, bora hata niangalie mpira wa Manchester city kuliko kuiangalia Manchester ya Mourinho" alisema Van Gaa.
"yani ni bora niangalie Manchester city ya Guardiola kuliko Manchester united ya Mourinho" aliongeza Van Gaal.
Mourinho alishawai kuwa chini ya Van Gaal kipindi cha mwaka 1996 mpaka mwaka 2000 wakati huo Pep Guardiola akiwa kama nahodha akatika klabu ya Barcelona.
"Man utd ya Mourinho inalinda sana lango lake kuliko Man utd yangu (Van Gaal), ukitaka kuamini hilo angalia kipindi changu timu pinzani zilikuwa zinalinda lango lao sana kuliko sasa hivi hazifanyi hivyo maana Man utd ya sasa inakaba sana" alimalizia Van Gaal
Post a Comment
Post a Comment