Mara baada ya wananchi wa nchi ya Kenya kufanya maandamano ya amani wakiwa na mabango ya kumuombea nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Victor Wayama ambaye ni raia wa Kenya na nahodha wa timu ya taifa ya nchini humo ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu, sasa maombi yao yamejibiwa.
Maombi ya wakenya hao yamejibiwa mara baada ya nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji kurejea mazoezini klabuni kwake Tottenham akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza mara baada ya kukaa nje kwa miezi minne.
Victor Wanyama ambaye alishafikaga nchini Tanzania na kushiriki katika mashindano yanayoendesahwa na chombo cha habari cha Clouds Media yanayoitwa Ndondo Cup akiwa kama mgeni rasmi ameanza mazoezi rasmi na kuwapa matumaini wakenya na watanzania na hata nchi za Afrika Mashariki akiwa kama mchezaji wa kwanza kutokea Afrika Mashariki kucheza katika ligi kuu Uingereza.
Post a Comment
Post a Comment