Mara baada ya kupokea vipigo mfululizo, kutoka kwenye ligi wikiendi iliyopita na kutoka kwa Bayern Munich katika klabu bingwa, klabu ya PSG imerudi kwenye makali yake kwa kupata ushindi jioni ya leo ikiifunga klabu ya Lille kwa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu.
PSG ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli, Angel Di Maria akifungua karamu hiyo ya magoli kabla ya kutoa pasi ya goli la pili akimpasia Pastore aliyefunga goli hilo na mwisho Kylian Mbappe akafunga goli la tatu na kuifanya PSG kuwa klabu ya kwanza kufikisha idadi kubwa ya magoli kwa bara la Ulaya katika michuano ya ligi. Ambapo katika michezo 17 imeshafunga magoli 51. Huku ikimwacha mtu wa pili kwa alama 12.
PSG ilicheza mchezo huo bila nyota wake Neymar Jr. ambaye anatumikia adhabu ya kukaa nje kwa michezo mitatu kutokana na kupata kadi nyekundu.
Michezo mingine Ligue 1;
Angers vs Montpellier
Guingamp vs Dijon
Metz vs Rennes
AS Monaco vs Troyes
Toulouse vs Caen
(michezo yote ni saa 22:00)
Post a Comment
Post a Comment