Kwa wapenzi wa soka waliojitokeza siku ile ya mechi ya kufuzu fainali za kombe la dunia chini ya miaka 17,  ambapo mechi iliisha kwa Tanzania kushinda kwa mabao 3-2. Bila shaka walikoshwa sana na kiwango cha yule kinda aliyefanya vyema siku kwa kuifungia Tanzania mabao mawili,  Yohana Oscar Mkomola ambaye alicheza vizuri na alikuwa kwenye kiwango kizuri sana siku iyo.
Jina lake kamili ni Yohana Oscar Mkomola,  aliyezaliwa mwezi july mwaka 2000.  Ni mtoto wa mwisho katika familia yao ambayo kwa sasa anaishi na mama yake pekee ambapo miaka kadhaa alimpoteza baba yake.  Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Mtoni Sabasaba kuanzia mwaka 2004 mpaka mwaka 2010 iliyopo Dar es Salaam na alianza safari yake ya kisoka akiichezea timu ya Emima ya uwanja wa Sifa hukohuko Mtoni Sabasaba. Na kwa sasa anaichezea pia klabu ya Azam B ambapo alijiungaunga na timu hiyo mwaka 2015.
Huo ni muhtasari kwa ufupi kuhusu nyota huyo ambaye wananchi wengi siku hiyo waliokuwa uwanja wa taifa walimtabiria makubwa kutokana na ufundi wake katika soka.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.