Hatimaye leo imetimia, kwa mara ya kwanza klabu ya PSG inapata kipigo chake cha kwanza katika ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
Tena imepokea kipigo huku ikiwa na wachezaji wake ghali zaidi, Neymar pamoja na Kylian Mbappe wakiongoza safu ya ushambuliaji ya PSG huku Edinson Cavani akianzia benchi kabla ya kuingia kuchukua nafasi ya Angel di Maria.
PSG imepokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa klabu ya Strasbough uku goli la PSG likifungwa na Kylian Mbappe akipokea pasi ya Rabiot.
Hichi kinakuwa kipigo cha kwanza katika ligi kuu Ufaransa ilichokikumba PSG ingawa bado haijabadili msimamo wa ligi kuu nchini umo.
Matokeo ya Ligue 1;
AS Monaco 1-0 Angers
OGC Nice 3-1 Metz
Post a Comment
Post a Comment