Usiku wa leo kutakuwa na michezo ya ligi kuu Uingereza ambapo vinara wa ligi hiyo, Manchester city wakishuka dimbani kumenyana na Swansea katika uwanja wa Liberty stadium. Swansea wakiwa nyumbani.
Licha ya umuhimu wa ushindi kwa Manchester city katika mchezo huu, lakini pia ushindi katika mchezo huu utaifanya klabu hiyo ya Manchester city iliyochini ya mhispania Pep Guardiola kuweka rekodi ya kuwa klabu iliyoshinda michezo mingi kwa msimu mmoja, ikiipiku rekodi iliyowekwa na Arsenal kwa kushinda michezo 14 msimu wa 2002.
Manchester city yenye alama 46 kwenye ligi kuu, itataka kushinda mchezo huu ili ipande zaidi na kuzidisha utofauti wa alama baina yake na Manchester united inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 35 sawa na Chelsea.
Manchester city itakaribishwa Liberty stadium usiku huu mida ya saa 22:45
Michezo mingine EPL;
Manchester united vs Bournemouth
West Ham vs Arsenal
Newcastle vs Everton
Southampton vs Leicester
Liverpool vs West Brom
Tottenham vs Brighton
Matokeo ya jana EPL;
Huddersfield 1-3 Chelsea
Burnley 1-0 Stoke city
Crystal Palace 1-1 Watford
Post a Comment
Post a Comment