Kiungo mkongwe wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Andres Iniesta amekiri kuwa anaogopa sana endapo nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye kwa sasa anaichezea PSG, Neymar Jr atajiunga na Real Madrid.

Neymar aliondoka Barcelona kwa dau lililovunja rekodi ya usajili duniani akitoka Barca kujiunga na PSG kwa kiasi cha paundi milioni 198 ametajwa kujiunga na Real Madrid ambao ni wapinzani wa Barcelona katika ligi kuu Hispania.

"naujua ubora na upekee wa Neymar, nahofia kama atajiunga na Real Madrid itamaanisha watakuwa wamempata nyota wa pekee na watakuwa wameongeza nguvu katika kikosi chao kutokana na upekee wake. Nami sitaki hilo litokee. Lakini mwisho wa siku kwenye mpira chochote kinaweza kutokea" alisema Iniesta

Neymar anatajwa kuhusishwa kujiunga na Real Madrid huku kukiwa na taarifa zikieleza kuwa nyota huyo anaonekana kutokuwa na furaha klabuni PSG.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.