Nadhani ushakutana na vituko vingi katika soka, lakini kituko hiki kinaweza kuwa kituko cha kufungia mwaka 2017 kikiwa kimetokea uko nchini Italia.
Siku ya jumatatu, Lazio ilishuka dimbani kwao jijini Roma kumenyana na Torino ambapo katika mchezo huo Lazio iliyokuwa nyumbani walifungwa 1-3 na wageni Torino ambapo mshambuliaji muhimu wa Lazio, Ciro Immobile alipewa kadi nyekundu, tukio ambalo mashabiki wa Lazio walililaani sana. Kadi hiyo alipewa na mwamuzi Pierro Giacomelli.
Siku ya jumanne, ikagundulika kuwa yule mwamuzi wa mchezo huo anamiliki mgahawa katika jiji la Roma ambapo ndipo yalipo makao ya Lazio. Basi mashabiki wa Lazio kupitia mitandao wakahamasishana na kuanza kuupigia kura mgahawa huo kwamba unatoa huduma mbovu na haufai.
Sasa nikuchekeshe? siku ya jumatano ambayo ndiyo leo, serikali ya nchini Italia kupitia jiji la Roma imeishusha thamani mgahawa huo mpaka kufikia nyota 1.
Mashabiki wa Lazio wamelipiza hasira zao, ndio ule msemo wa Kiswahili, ukisema unajua hivi, basi mi najua vile.
Umeionaje hiyo? toa maoni yako.
Post a Comment
Post a Comment