Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameongelea uwezekano wa nyota wake, Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao mkataba wao unaisha mwezi juni mwakani.

Kumekuwa na tetesi kwa Mesut Ozil kutakiwa na klabu kubwa ambapo Barcelona imekuwa ikitajwa kumsajili kama mbadala endapo ikimkosa Phillip Coutinho wa Liverpool wakati Alexis Sanchez amekuwa akihusishwa kwa karibu kujiunga na Manchester city lakini pia PSG ikiwemo.

Akizungumzia tetesi hizo kocha Arsene Wenger amesema "wote wataendelea kuwepo, hata mi napenda kuwaona wakisalia Arsenal, sioni wakiondoka Arsenal" alisema kocha huyo raia wa Ufaransa.

Kwa madai ya kocha Arsene Wenger anadai hakuna mchezaji anayeondoka.

Arsenal itamenyana na Newcastle katika raundi ya 18 wiki hii ambapo imeporomoka kutoka nafasi iliyokuwepo (nafasi ya 5) mpaka kufikia nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza, huku akiachwa alama 19 na Manchester city iliyoko kileleni.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.