Chama cha soka nchini Uingereza, FA kupitia kwa msemaji wa chama hicho ametuma taarifa ya kufanyika uchunguzi wa maneno aliyoyatamka kocha wa klabu ya nchini humo Manchester united, Jose Mourinho kabla ya kuanza kwa mchezo wa timu hiyo dhidi ya Manchester city jumapili iliyopita, na Man city walishinda 2-1.
Kabla ya mchezo huo, kulifanyika mahojiano na kocha wa Manchester united, Mourinho ambapo inaelezwa chama cha soka nchini humo ina wasiwasi na maneno hayo na wanamtaka Mourinho akatoe ufafanuzi juu ya maneno hayo ambapo inaelezwa pia aliingizia maneno ya kuongelea siasa ya mzozo wa jimbo la Cataluna anapotokea kocha wa Man city, Pep Guardiola ambapo jimbo hilo linadai uhuru likitaka kujitenga na nchi ya Hispania.
FA wamemwambia Mourinho anatakiwa aripoti kwenye chama hicho mpaka mwisho tarehe 18 ya mwezi desemba, na akishindwa kufika basi yatamkuta makubwa.
Post a Comment
Post a Comment