Labda umekuwa ukishangazwa na magoli ya mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata aliyesajiliwa akitokea Real Madrid ya nchini Hispania, amekuwa akifunga sana kwa kutumia kichwa.
Ushawai kujiuliza kwanini nyota huyo anafunga sana kwa kutumia kichwa?
Sababu ni hii,
Akihojiwa na jarida la Chelsea, Morata alisema "wakati nilipokuwa mdogo, nikiwa nafanya mazoezi na baba alikuwa akinifundisha sana kupiga mipira kwa kichwa. Muda mwengine alikuwa ananipasia pale tu naporuka juu na kunitaka nipige kwa kutumia kichwa, na kwa kuwa nilikuwa mtoto, nilikuwa najisikia vizuri kuruka juu. Nadhani hiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa kunifanya niwe vizuri kwa mipira ya vichwa" alifichua Morata
Morata mpaka sasa ameshaifungia Chelsea magoli zaidi ya 6 kwa kichwa.
Lakini pia nyota huyo amekiri kuwa huwa anajifunza mengi kupitia nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba. "tangu nimefika Chelsea nimekuwa namtazama Drogba haswa nikiwa nyumbani kupitia DVD na kujifunza mengi kupitia yeye" aliongeza Morata.
Post a Comment
Post a Comment